Skip to content
Habakuki 3:3-15

Habakuki 3:3-15

3
Mungu alitoka Temani, yeye Aliye Mtakatifu kutoka Mlima Parani. Utukufu wake ulifunika mbingu, na sifa zake zikaifunika dunia.
4
Mngʼao wake ulikuwa kama jua lichomozalo; mionzi ilimulika kutoka mkononi mwake, ambako nguvu zake zilifichwa.
5
Tauni ilimtangulia; maradhi ya kuambukiza yalifuata nyayo zake.
6
Alisimama, akaitikisa dunia; alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke. Milima ya zamani iligeuka mavumbi na vilima vilivyozeeka vikaanguka. Njia zake ni za milele.
7
Niliona watu wa Kushani katika dhiki, na makazi ya Midiani katika maumivu makali.
8
Ee Bwana, uliikasirikia mito? Je, ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya vijito? Je, ulighadhibikia bahari ulipoendesha farasi wako na magari yako ya ushindi?
9
Uliufunua upinde wako na kuita mishale mingi. Uliigawa dunia kwa mito;
10
milima ilikuona ikatetemeka. Mafuriko ya maji yakapita huko; vilindi vilinguruma na kuinua mawimbi yake juu.
11
Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni katika mngʼao wa mishale yako inayoruka, na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao.
12
Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia, na katika hasira ulikanyaga mataifa.
13
Ulikuja kuwaokoa watu wako, kumwokoa uliyemtia mafuta. Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu, ukamvua toka kichwani hadi wayo.
14
Kwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya, wakifurahi kama walio karibu kutafuna wale wanyonge waliokuwa mafichoni.
15
Ulikanyaga bahari kwa farasi wako, ukisukasuka maji makuu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options