Mwanzo 5:25-29
25
Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki.
26
Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
27
Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.
28
Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
29
Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.”
Settings