Mwanzo 10:11-24
11
Kutoka nchi ile alikwenda Ashuru, ambako alijenga Ninawi, Rehoboth-iri, Kala,
12
na Reseni, iliyo kati ya Ninawi na Kala; huo ndio mji mkubwa.
13
Misraimu alikuwa baba wa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
14
Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti), na Wakaftori.
15
Kanaani alikuwa baba wa: Sidoni mzaliwa wake wa kwanza, Hethi,
16
Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,
17
Wahivi, Waariki, Wasini,
18
Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Baadaye koo za Wakanaani zilitawanyika,
19
na mipaka ya Kanaani ilienea kutoka Sidoni kuelekea Gerari hadi Gaza, kisha kuelekea Sodoma, Gomora, Adma na Seboimu, hadi kufikia Lasha.
20
Hawa ni wana wa Hamu kwa koo zao na lugha zao, katika nchi zao na mataifa yao.
21
Shemu ambaye ni ndugu mkubwa wa Yafethi, kwake kulizaliwa wana pia. Shemu alikuwa baba wa wana wote wa Eberi.
22
Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.
23
Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mesheki.
24
Arfaksadi alikuwa baba wa Shela, naye Shela akamzaa Eberi.
Settings