Skip to content
Wagalatia 1:11-24

Wagalatia 1:11-24

11
Ndugu zangu, nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana na wanadamu.
12
Kwa maana mimi sikuipokea hiyo Injili kutoka kwa mwanadamu, wala sikufundishwa na mtu, bali niliipata kwa ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo.
13
Ninyi mmekwisha kusikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu kwa nguvu na kujaribu kuliangamiza.
14
Nami niliendelea sana katika dini ya Kiyahudi kuliko Wayahudi wengi wa rika yangu maana nilijitahidi sana katika desturi za baba zangu.
15
Lakini ilipompendeza Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu na kuniita kwa neema yake,
16
alimdhihirisha Mwanawe kwangu, ili nipate kumhubiri miongoni mwa watu wa Mataifa. Mimi sikushauriana na mwanadamu yeyote,
17
wala sikupanda kwenda Yerusalemu kuwaona hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda mara moja Arabuni na kisha nikarudi Dameski.
18
Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kuonana na Kefa na nilikaa naye siku kumi na tano.
19
Lakini sikumwona mtume mwingine yeyote isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana.
20
Nawahakikishia mbele za Mungu kuwa ninayowaandikia si uongo.
21
Baadaye nilikwenda sehemu za Syria na Kilikia.
22
Lakini mimi binafsi sikujulikana kwa makanisa ya huko Uyahudi yaliyo katika Kristo.
23
Wao walisikia habari tu kwamba, “Mtu yule ambaye hapo kwanza alikuwa akitutesa sasa anahubiri imani ile ile aliyokuwa akijaribu kuiangamiza.”
24
Nao wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options