2 Timotheo 4:9-15
9
Jitahidi kuja kwangu upesi
10
kwa sababu Dema, kwa kuupenda ulimwengu, ameniacha na amekwenda Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia na Tito amekwenda Dalmatia.
11
Ni Luka peke yake aliye hapa pamoja nami. Mtafute Marko uje naye kwa sababu ananifaa sana katika huduma yangu.
12
Nimemtuma Tikiko huko Efeso.
13
Utakapokuja, niletee lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa na vile vitabu vyangu, hasa vile vya ngozi.
14
Aleksanda yule mfua chuma alinitendea ubaya mkubwa. Bwana atamlipa kwa ajili ya yale aliyotenda.
15
Wewe pia ujihadhari naye kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu.
Settings