1 Wafalme 16:24-33
24
Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbili za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.
25
Lakini Omri akatenda maovu machoni pa Bwana na kutenda dhambi kuliko wote waliomtangulia.
26
Akaenenda katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake, ambazo alisababisha Israeli kutenda, hivyo basi wakamkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.
27
Kwa matukio mengine ya utawala wa Omri, yale aliyofanya na vitu alivyovifanikisha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
28
Omri akalala pamoja na baba zake na akazikwa huko Samaria. Ahabu mwanawe akatawala mahali pake.
29
Katika mwaka wa thelathini na nane wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala Israeli akiwa Samaria kwa miaka ishirini na miwili.
30
Ahabu mwana wa Omri akafanya maovu zaidi machoni mwa Bwana kuliko yeyote aliyewatangulia.
31
Kama vile haikutosha kuishi kama Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti wa Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, naye akaanza kumtumikia Baali na kumwabudu.
32
Akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali katika hekalu la Baali lile alilolijenga huko Samaria.
33
Pia Ahabu akatengeneza nguzo ya Ashera na kufanya mengi ili kumkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko walivyofanya wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.
Settings