Skip to content
1 Wafalme 16:21-28

1 Wafalme 16:21-28

21
Ndipo watu wa Israeli wakagawanyika katika makundi mawili, nusu wakamuunga mkono Tibni mwana wa Ginathi ili awe mfalme na nusu nyingine wakamuunga mkono Omri.
22
Lakini wafuasi wa Omri wakajionyesha wenye nguvu kuliko wale wa Tibni mwana wa Ginathi. Hivyo Tibni akafa na Omri akawa mfalme.
23
Katika mwaka wa thelathini na moja wa utawala wa Asa mfalme wa Yuda, Omri akawa mfalme wa Israeli, naye akatawala kwa miaka kumi na miwili, sita kati ya hiyo katika Tirsa.
24
Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta mbili za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.
25
Lakini Omri akatenda maovu machoni pa Bwana na kutenda dhambi kuliko wote waliomtangulia.
26
Akaenenda katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake, ambazo alisababisha Israeli kutenda, hivyo basi wakamkasirisha Bwana, Mungu wa Israeli kwa sanamu zao zisizofaa.
27
Kwa matukio mengine ya utawala wa Omri, yale aliyofanya na vitu alivyovifanikisha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Israeli?
28
Omri akalala pamoja na baba zake na akazikwa huko Samaria. Ahabu mwanawe akatawala mahali pake.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options