1 Wafalme 15:1-8
1
Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya akawa mfalme wa Yuda,
2
naye akatawala huko Yerusalemu miaka mitatu. Mama yake aliitwa Maaka binti Abishalomu.
3
Alitenda dhambi zote baba yake alizotenda kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana Mungu wake kama moyo wa Daudi baba yake ulivyokuwa.
4
Pamoja na hayo, kwa ajili ya Daudi, Bwana Mungu wake akampa taa katika Yerusalemu kwa kumwinua mwana atawale badala yake na kwa kuifanya Yerusalemu kuwa imara.
5
Kwa kuwa Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana na hakushindwa kushika maagizo yote ya Bwana siku zote za uhai wake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti.
6
Kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu wakati wote wa maisha ya Abiya.
7
Kwa habari ya matukio mengine ya utawala wa Abiya na yote aliyofanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Yuda? Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.
8
Naye Abiya akalala na baba zake akazikwa katika Mji wa Daudi. Asa mwanawe akawa mfalme baada yake.
Settings