Zaburi54
Listen to this chapter
0:00
0:00
Maombi ya Daudi Katika Dhiki
1
Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Wakati Wazifu walimwendea Sauli na kumjulisha, “Je, Daudi hajifichi miongoni mwetu?” Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako.
2
Ee Mungu, sikia maombi yangu, usikilize maneno ya kinywa changu.
3
Wageni wananishambulia, watu wakatili wanayatafuta maisha yangu, watu wasiomjali Mungu.
Uhakikisho wa Msaada wa Mungu
4
Hakika Mungu ni msaada wangu, Bwana ndiye anayenitegemeza.
5
Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize.
Nadhiri ya Sifa na Shukrani
6
Nitakutolea dhabihu za hiari; Ee Bwana, nitalisifu jina lako kwa kuwa ni vyema.
7
Kwa maana ameniokoa katika shida zangu zote, na macho yangu yamewatazama adui zangu kwa ushindi.
Use ← → arrow keys to navigate
Settings
Reading Style
Typeface
Font Size px
Reading Width chars
Options
Study Note