Rukia maudhui

Zaburi20

Maombi ya Wokovu wa Mfalme

1
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Bwana na akujibu unapokuwa katika dhiki, jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.
2
Na akutumie msaada kutoka patakatifu na akupatie msaada kutoka Sayuni.
3
Na azikumbuke dhabihu zako zote, na azikubali sadaka zako za kuteketezwa.
4
Na akujalie haja ya moyo wako, na aifanikishe mipango yako yote.
5
Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda, tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu. Bwana na akupe haja zako zote.

Tamko la Kumtumaini Mungu

6
Sasa nafahamu kuwa Bwana humwokoa mpakwa mafuta wake, humjibu kutoka mbingu yake takatifu kwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.

Kulitumaini Jina la Bwana

7
Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi, bali sisi tutalitumainia jina la Bwana, Mungu wetu.
8
Wao wameshushwa chini na kuanguka, bali sisi tunainuka na kusimama imara.

Ombi la Mwisho la Wokovu wa Mfalme

9
Ee Bwana, mwokoe mfalme! Tujibu tunapokuita!
Use arrow keys to navigate
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options