Rukia maudhui

Zaburi128

Baraka za Kumcha BWANA

1
Wimbo wa kwenda juu. Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake.
2
Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

Ufanisi Nyumbani na Katika Familia

3
Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako.
4
Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana.

Baraka Kutoka Sayuni na kwa Israeli

5
Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu,
6
nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.
Use arrow keys to navigate
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options