Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Death of the Wicked

11 mistari · 20 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na mmoja.

  2. Alifanya maovu machoni pa Bwana Mungu wake, wala hakujinyenyekeza mbele ya nabii Yeremia, ambaye alinena neno la Bwana.

  3. Pia alimwasi Mfalme Nebukadneza, ambaye alikuwa amemwapisha kwa jina la Mungu. Akashupaza shingo na akafanya moyo wake kuwa mgumu wala hakutaka kumgeukia Bwana, Mungu wa Israeli.

  4. Vitisho vimemtia hofu kila upande, na adui zake humwandama kila hatua.

  5. Janga linamwonea shauku; maafa yako tayari kwa ajili yake aangukapo.

  6. Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake.

  7. Atangʼolewa kutoka usalama wa hema lake, na kupelekwa kwa mfalme wa vitisho.

  8. Moto utakaa katika hema lake; moto wa kiberiti utamwagwa juu ya makao yake.

  9. Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka.

  10. Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku.

  11. Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake.