Mistari ya Biblia kuhusu The Church: The wicked persecute
Mistari kuhusu The wicked persecute
Naye Sauli alikuwepo pale, akiridhia kuuawa kwa Stefano. Siku ile kukatukia mateso makuu dhidi ya kanisa huko Yerusalemu, waumini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia Uyahudi na Samaria.
Watu wacha Mungu wakamzika Stefano na kumwombolezea sana.
Lakini kwa habari ya Sauli alikuwa analiharibu kanisa, akiingia nyumba kwa nyumba, akiwaburuta wanawake na wanaume na kuwatupa gerezani.