Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Rashness: General references

8 mistari · 1 kipengele

Mistari kuhusu General references

  1. Katika taabu yangu nilisema, “Wanadamu wote ni waongo.”

  2. Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi, bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu.

  3. Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa, wala kufanya haraka na kuikosa njia.

  4. Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida, kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini.

  5. usiharakishe kukipeleka mahakamani, maana utafanya nini mwishoni kama jirani yako atakuaibisha?

  6. Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye.

  7. Usiwe mwepesi kuzungumza, usiwe na haraka katika moyo wako kuzungumza lolote mbele za Mungu. Mungu yuko mbinguni nawe uko duniani, kwa hiyo maneno yako na yawe machache.

  8. Usiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako, kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.