Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Longevity

13 mistari · 2 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

  1. Basi Mungu akamwambia, “Kwa kuwa umeomba neno hili na hukuomba maisha marefu au upate utajiri kwa nafsi yako, wala adui zako wafe, bali umeomba ufahamu katika kutoa haki,

  2. nitafanya lile uliloomba. Nitakupa moyo wa hekima na wa ufahamu, kiasi kwamba hajakuwepo mtu mwingine kama wewe, wala kamwe hatakuwepo baada yako.

  3. Zaidi ya hayo, nitakupa yale ambayo hukuomba, yaani utajiri na heshima, ili kwamba maisha yako yote hapatakuwa na mtu kama wewe miongoni mwa wafalme.

  4. Nawe kama ukienenda katika njia zangu na kutii sheria na amri zangu kama baba yako Daudi alivyofanya, nitakupa maisha marefu.”

  5. Njooni, watoto wangu, mnisikilize, nitawafundisha kumcha Bwana.

  6. Yeyote kati yenu anayependa uzima na kutamani kuziona siku nyingi njema,

  7. basi auzuie ulimi wake na mabaya, na midomo yake kutokana na kusema uongo.

  8. Mwanangu, usisahau mafundisho yangu, bali zitunze amri zangu moyoni mwako,

  9. kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako na kukuletea mafanikio.

  10. Tena alikuwako Hekaluni nabii mmoja mwanamke, jina lake Ana binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa mzee sana; naye alikuwa ameolewa na kuishi na mume kwa miaka saba tu, kisha mumewe akafa.

  11. Hivyo alikuwa mjane na umri wake ulikuwa miaka themanini na minne. Yeye hakuondoka humo Hekaluni usiku wala mchana, bali alikuwa akimwabudu Mungu, akifunga na kuomba.

  12. Kwa maana, “Yeyote apendaye uzima na kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila.

  13. Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema; lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.