Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Kings: Rendered hereditary in the family of David

8 mistari · 175 vipengele

Mistari kuhusu Rendered hereditary in the family of David

  1. Siku zako zitakapokwisha nawe ulale pamoja na baba zako, nitainua mzao wako aingie mahali pako, ambaye atatoka viunoni mwako, nami nitauimarisha ufalme wake.

  2. Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, nami nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele.

  3. Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Atakapokosea nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu, kwa adhabu ya kupigwa na wanadamu.

  4. Lakini upendo wangu kamwe hautaondolewa kwake, kama nilivyouondoa kwa Sauli, niliyemwondoa atoke mbele yako.

  5. Nyumba yako na ufalme wako utadumu milele mbele zangu, kiti chako cha enzi kitafanywa imara milele.’ ”

  6. Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu, nami sitamdanganya Daudi:

  7. kwamba uzao wake utaendelea milele, na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua;

  8. kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu angani.”