Skip to content
Zekaria 2:1-5

Maono ya Kamba ya Kupimia

Zekaria 2:1-5
1
Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake!
2
Nikamuuliza, “Unakwenda wapi?” Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.”
3
Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye
4
na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo.
5
Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema Bwana, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 90 chars

Options