Wimbo 7:10
Inaonyesha mstari 10 pamoja na muktadha unaouzunguka.
7
Umbo lako ni kama la mtende, nayo matiti yako kama vishada vya matunda.
8
Nilisema, “Nitakwea mtende, nami nitayashika matunda yake.” Matiti yako na yawe kama vishada vya mzabibu, harufu nzuri ya pumzi yako kama matofaa,
9
na kinywa chako kama divai bora kuliko zote. Mpendwa Divai na iende moja kwa moja hadi kwa mpenzi wangu, ikitiririka polepole juu ya midomo na meno.
10
Mimi ni mali ya mpenzi wangu, nayo shauku yake ni juu yangu.
11
Njoo, mpenzi wangu, twende mashambani, twende tukalale huko vijijini.
12
Hebu na twende mapema katika mashamba ya mizabibu tuone kama mizabibu imechipua, kama maua yake yamefunguka, na kama mikomamanga imetoa maua: huko nitakupa penzi langu.
13
Mitunguja hutoa harufu zake nzuri, kwenye milango yetu kuna matunda mazuri, mapya na ya zamani, ambayo nimekuhifadhia wewe, mpenzi wangu.
Settings