Warumi 16:25
Inaonyesha mstari 25 pamoja na muktadha unaouzunguka.
22
Mimi, Tertio, niliye mwandishi wa waraka huu, nawasalimu katika Bwana.
23
Gayo, ambaye ni mwenyeji wangu na wa kanisa lote, anawasalimu. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto ndugu yetu pia wanawasalimu. [
24
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amen.]
25
Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya ninyi imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Yesu Kristo, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale.
26
Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii
27
Mungu aliye pekee, mwenye hekima, ambaye kwa njia ya Yesu Kristo utukufu ni wake milele na milele! Amen.
Settings