Zaburi 88:3-7
3
Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, na maisha yangu yanakaribia kaburi.
4
Nimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni, niko kama mtu asiye na nguvu.
5
Nimetengwa pamoja na wafu, kama waliochinjwa walalao kaburini, ambao huwakumbuki tena, ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako.
6
Umenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana, katika vina vya giza nene.
7
Ghadhabu yako imekuwa nzito juu yangu, umenigharikisha kwa mawimbi yako yote.
Settings