Zum Inhalt springen
Zaburi 73:17-26

Zaburi 73:17-26

17
Mpaka nilipoingia patakatifu pa Mungu, ndipo nilipotambua mwisho wao.
18
Hakika unawaweka mahali pa utelezi, unawaangusha chini kwa uharibifu.
19
Tazama jinsi wanavyoangamizwa ghafula, wanatoweshwa kabisa na vitisho!
20
Kama ndoto mtu aamkapo, hivyo wakati uinukapo, Ee Bwana, utawatowesha kama ndoto.
21
Wakati moyo wangu ulipohuzunishwa, na roho yangu ilipotiwa uchungu,
22
nilikuwa mpumbavu na mjinga, nilikuwa mnyama mkatili mbele yako.
23
Hata hivyo niko pamoja nawe siku zote, umenishika mkono wangu wa kuume.
24
Unaniongoza kwa shauri lako, hatimaye utaniingiza katika utukufu.
25
Nani niliye naye mbinguni ila wewe? Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.
26
Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa, bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu na fungu langu milele.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options