Zaburi 72:4-14
4
Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu.
5
Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote.
6
Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanyeshayo ardhi.
7
Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma.
8
Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto mpaka miisho ya dunia.
9
Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi.
10
Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi.
11
Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia.
12
Kwa maana atamwokoa mhitaji anayemlilia, aliyeonewa asiye na wa kumsaidia.
13
Atawahurumia wanyonge na wahitaji na kuwaokoa wahitaji kutoka mauti.
14
Atawaokoa kutoka uonevu na ukatili, kwani damu yao ni ya thamani machoni pake.
Settings