Zaburi 64:1-6
1
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, unisikie ninapoeleza lalamiko langu, uyahifadhi maisha yangu kutokana na vitisho vya adui.
2
Unifiche kutokana na shauri la siri la waovu, kutokana na zile kelele za kundi la watenda mabaya.
3
Wananoa ndimi zao kama panga na kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha.
4
Hurusha mishale kutoka kwenye mavizio kwa mtu asiye na hatia, humrushia ghafula bila woga.
5
Kila mmoja humtia moyo mwenzake katika mipango mibaya; huzungumza juu ya kuficha mitego yao, nao husema, “Ni nani ataiona?”
6
Hufanya shauri baya la dhuluma na kusema, “Tumebuni mpango mkamilifu!” Hakika nia na moyo wa mwanadamu vina hila.
Settings