Skip to content
Zaburi 40:11-17

Zaburi 40:11-17

11
Ee Bwana, usizuilie huruma zako, upendo wako na kweli yako daima vinilinde.
12
Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka, dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona. Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu, nao moyo unazimia ndani yangu.
13
Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa; Ee Bwana, njoo hima unisaidie.
14
Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu, waaibishwe na kufadhaishwa; wote wanaotamani kuangamizwa kwangu, warudishwe nyuma kwa aibu.
15
Wale waniambiao, “Aha! Aha!” wafadhaishwe na iwe aibu yao.
16
Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Bwana atukuzwe!”
17
Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji; Bwana na anifikirie. Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu; Ee Mungu wangu, usikawie.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options