Skip to content
Zaburi 29:3-9

Zaburi 29:3-9

3
Sauti ya Bwana iko juu ya maji; Mungu wa utukufu hupiga radi, Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.
4
Sauti ya Bwana ina nguvu; sauti ya Bwana ni tukufu.
5
Sauti ya Bwana huvunja mierezi; Bwana huvunja vipande vipande mierezi ya Lebanoni.
6
Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama, Sirioni urukaruke kama mwana nyati.
7
Sauti ya Bwana hupiga kwa miali ya umeme wa radi.
8
Sauti ya Bwana hutikisa jangwa; Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi.
9
Sauti ya Bwana huzalisha ayala, na huuacha msitu wazi. Hekaluni mwake wote wasema, “Utukufu!”
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options