Zaburi 119:169-176
169
Ee Bwana, kilio changu na kifike mbele zako, nipe ufahamu sawasawa na neno lako.
170
Maombi yangu na yafike mbele zako, niokoe sawasawa na ahadi yako.
171
Midomo yangu na ibubujike sifa, kwa kuwa unanifundisha maagizo yako.
172
Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako, kwa kuwa amri zako zote ni za haki.
173
Mkono wako uwe tayari kunisaidia, kwa kuwa nimechagua mausia yako.
174
Ee Bwana, ninatamani wokovu wako, na sheria yako ni furaha yangu.
175
Nijalie kuishi ili nipate kukusifu, na sheria zako zinitegemeze.
176
Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea. Mtafute mtumishi wako, kwa kuwa sijasahau amri zako.
Settings