Zaburi 119:153-160
153
Yaangalie mateso yangu, uniokoe, kwa kuwa sijasahau sheria yako.
154
Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako.
155
Wokovu uko mbali na waovu, kwa kuwa hawatafuti maagizo yako.
156
Ee Bwana, huruma zako ni kuu, uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako.
157
Adui wanaonitesa ni wengi, lakini mimi sitaziacha sheria zako.
158
Ninawatazama wasioamini kwa chuki, kwa kuwa hawalitii neno lako.
159
Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako; Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako.
160
Maneno yako yote ni kweli, sheria zako zote za haki ni za milele.
Settings