Skip to content
Mithali 6:26-35

Mithali 6:26-35

26
kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini, hata ukose kipande cha mkate, naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa.
27
Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake bila nguo zake kuungua?
28
Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka bila miguu yake kuungua?
29
Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine; hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.
30
Watu hawamdharau mwizi kama akiiba kukidhi njaa yake wakati ana njaa.
31
Pamoja na hayo, kama akikamatwa, lazima alipe mara saba, ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake.
32
Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa; yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.
33
Mapigo na aibu ni fungu lake na aibu yake haitafutika kamwe;
34
kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume, naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi.
35
Hatakubali fidia yoyote; atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options