Mithali 6:24-28
24
yakikulinda na mwanamke aliyepotoka, kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.
25
Moyo wako usitamani uzuri wake wala macho yake yasikuteke,
26
kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini, hata ukose kipande cha mkate, naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa.
27
Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake bila nguo zake kuungua?
28
Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka bila miguu yake kuungua?
Settings