Mithali 16:1-9
1
Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa Bwana.
2
Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na Bwana.
3
Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa.
4
Bwana hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi.
5
Bwana huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa.
6
Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya.
7
Njia za mtu zinapompendeza Bwana, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani.
8
Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu.
9
Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Bwana huelekeza hatua zake.
Settings