Skip to content
Mithali 10:22-32

Mithali 10:22-32

22
Baraka ya Bwana hutajirisha, wala haichanganyi huzuni.
23
Mpumbavu hufurahia tabia mbaya, lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima.
24
Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata; kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa.
25
Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele.
26
Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma.
27
Kumcha Bwana huongeza urefu wa maisha, lakini miaka ya mwovu inafupishwa.
28
Tarajio la mwenye haki ni furaha, bali matumaini ya mwovu huwa si kitu.
29
Njia ya Bwana ni kimbilio kwa wenye haki, lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya.
30
Kamwe wenye haki hawataondolewa, bali waovu hawatasalia katika nchi.
31
Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima, bali ulimi wa upotovu utakatwa.
32
Midomo ya wenye haki inajua kile kinachofaa, bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options