Skip to content
Nehemia 12:12-26

Nehemia 12:12-26

12
Katika siku za Yoyakimu, kulikuwa na wakuu wa jamaa za kikuhani: wa jamaa ya Seraya, Meraya; wa jamaa ya Yeremia, Hanania;
13
wa jamaa ya Ezra, Meshulamu; wa jamaa ya Amaria, Yehohanani;
14
wa jamaa ya Maluki, Yonathani; wa jamaa ya Shebania, Yosefu;
15
wa jamaa ya Harimu, Adna; wa jamaa ya Meremothi, Helkai;
16
wa jamaa ya Ido, Zekaria; wa jamaa ya Ginethoni, Meshulamu;
17
wa jamaa ya Abiya, Zikri; wa jamaa ya Miniamini na ya Maazia, Piltai;
18
wa jamaa ya Bilgai, Shamua; wa jamaa ya Shemaya, Yehonathani;
19
wa jamaa ya Yoyaribu, Matenai; wa jamaa ya Yedaya, Uzi;
20
wa jamaa ya Salu, Kalai; wa jamaa ya Amoki, Eberi;
21
wa jamaa ya Hilkia, Hashabia; wa jamaa ya Yedaya, Nethaneli.
22
Wakuu wa jamaa za Walawi katika siku za Eliashibu, Yoyada, Yohanani na Yadua, pia wale jamaa za makuhani, waliandikishwa wakati wa utawala wa Dario, Mwajemi.
23
Wakuu wa jamaa miongoni mwa wazao wa Lawi hadi wakati wa Yohanani mwana wa Eliashibu waliandikishwa katika kitabu cha kumbukumbu.
24
Viongozi wa Walawi walikuwa: Hashabia, Sherebia, Yeshua mwana wa Kadmieli na wenzao, waliosimama mkabala nao kusifu na kushukuru, sehemu moja ikipokezana na nyingine kama ilivyoagizwa na Daudi mtu wa Mungu.
25
Mabawabu waliokuwa wakilinda kwenye malango ya ghala ni: Matania, Bakbukia, Obadia, Meshulamu, Talmoni na Akubu.
26
Walihudumu siku za Yoyakimu mwana wa Yeshua, mwana wa Yosadaki, na katika siku za mtawala Nehemia, na za Ezra kuhani na mwandishi.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options