Mathayo 21:14-19
14
Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya.
15
Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika.
16
Wakamuuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, “ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa’?”
17
Akawaacha, akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko.
18
Asubuhi na mapema, Yesu alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa.
19
Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka.
Settings