Waamuzi 5:3
Inaonyesha mstari 3 pamoja na muktadha unaouzunguka.
1
Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu:
2
“Wakuu katika Israeli wanapoongoza, wakati watu wanapojitoa kwa hiari yao wenyewe: mhimidini Bwana!
3
“Sikieni hili, enyi wafalme! Sikilizeni, enyi watawala! Nitamwimbia Bwana, nitaimba; kwa wimbo nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli.
4
“Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri, ulipopita katika mashamba ya Edomu, nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga, naam, mawingu yakamwaga maji.
5
Milima ilitetemeka mbele za Bwana, hata ule wa Sinai, mbele za Bwana, Mungu wa Israeli.
6
“Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi, katika siku za Yaeli, barabara kuu hazikuwa na watu; wasafiri walipita njia za kando.
Settings