Yohana 7:1-10
1
Baada ya mambo haya, Yesu alikwenda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Uyahudi kwa sababu Wayahudi huko walitaka kumuua.
2
Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
3
Hivyo ndugu zake Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende Uyahudi ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya.
4
Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri. Kama unafanya mambo haya, jionyeshe kwa ulimwengu.”
5
Hata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini.
6
Yesu akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote.
7
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu.
8
Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.”
9
Akiisha kusema hayo, akabaki Galilaya.
10
Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alikwenda lakini kwa siri.
Settings