Yohana 4:23-30
23
Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta.
24
Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
25
Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”
26
Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.”
27
Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”
28
Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu,
29
“Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Kristo?”
30
Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.
Settings