Yohana 4:27-38
27
Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au “Kwa nini unazungumza naye?”
28
Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini akawaambia watu,
29
“Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Kristo?”
30
Basi wakamiminika watu kutoka mjini wakamwendea Yesu.
31
Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Rabi, kula angalau chochote.”
32
Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”
33
Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?”
34
Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake.
35
Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune?’ Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa!
36
Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunaye wafurahi pamoja.
37
Hivyo kule kusema, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa.
38
Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda, wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”
Settings