Ayubu 8:11
Inaonyesha mstari 11 pamoja na muktadha unaouzunguka.
8
“Ukaulize vizazi vilivyotangulia na uone baba zao walijifunza nini,
9
kwa kuwa sisi tumezaliwa jana tu na hatujui lolote, nazo siku zetu duniani ni kama kivuli tu.
10
Je, hawatakufundisha na kukueleza? Je, hawataleta maneno kutoka kwenye kufahamu kwao?
11
Je, mafunjo yaweza kumea mahali pasipo na matope? Matete yaweza kustawi bila maji?
12
Wakati bado yanaendelea kukua kabla ya kukatwa, hunyauka haraka kuliko majani mengine.
13
Huu ndio mwisho wa watu wote wanaomsahau Mungu; vivyo hivyo matumaini ya wasiomjali Mungu huangamia.
14
Lile analolitumainia huvunjika upesi; lile analolitegemea ni utando wa buibui.
Settings