Skip to content
Ayubu 8:1-7

Bildadi amshutumu Ayubu na kuitetea haki ya Mungu

Ayubu 8:1-7
1
Kisha Bildadi Mshuhi akajibu:
2
“Hata lini wewe utasema mambo kama haya? Maneno yako ni kama upepo mkuu.
3
Je, Mungu hupotosha hukumu? Je, Mwenyezi hupotosha kile kilicho haki?
4
Watoto wako walipomtenda dhambi, aliwapa adhabu ya dhambi yao.
5
Lakini ukimtafuta Mungu, nawe ukamsihi Mwenyezi,
6
ikiwa wewe ni safi na mnyofu, hata sasa atainuka mwenyewe kwa niaba yako, na kukurudisha katika mahali pako pa haki.
7
Ijapokuwa mwanzo wako ulikuwa mdogo, lakini mwisho wako utakuwa wa mafanikio.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 90 chars

Options