Ayubu 20:4-11
4
“Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani, tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani,
5
macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi, nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu.
6
Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni na kichwa chake hugusa mawingu,
7
ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe. Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’
8
Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena, amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.
9
Jicho lililomwona halitamwona tena; mahali pake hapatamwona tena.
10
Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini, nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyangʼanya watu.
11
Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake, zitalala naye mavumbini.
Settings