Перейти до вмісту
Ayubu 20:10-22

Ayubu 20:10-22

10
Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini, nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyangʼanya watu.
11
Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake, zitalala naye mavumbini.
12
“Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake naye huuficha chini ya ulimi wake,
13
ingawa hawezi kukubali kuuachia uende, lakini huuweka kinywani mwake.
14
Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake, nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake.
15
Atatema mali alizozimeza; Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.
16
Atanyonya sumu za majoka; meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.
17
Hatafurahia vijito, mito inayotiririsha asali na siagi.
18
Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila; hatafurahia faida itokanayo na biashara yake.
19
Kwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu; amenyangʼanya kwa nguvu nyumba asizozijenga.
20
“Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana; hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake.
21
Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale; kufanikiwa kwake hakutadumu.
22
Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata; taabu itamjia kwa nguvu zote.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options