Ayubu 17:11-16
11
Siku zangu zimepita, mipango yangu imevunjika, vivyo hivyo shauku za moyo wangu.
12
Watu hawa hufanya usiku kuwa mchana, kwenye giza wao husema, ‘Mwanga u karibu.’
13
Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi, kama nikikitandika kitanda changu gizani,
14
kama nikiuambia uharibifu, ‘Wewe u baba yangu,’ na kuliambia buu, ‘Wewe u mama yangu’ au ‘Dada yangu,’
15
liko wapi basi tarajio langu? Ni nani awezaye kuona tarajio lolote kwa ajili yangu?
16
Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti? Je, tutashuka pamoja mavumbini?”
Settings