Yeremia 50:21-32
21
“Shambulieni nchi ya Merathaimu na wale waishio huko Pekodi. Wafuatieni, waueni na kuwaangamiza kabisa,” asema Bwana. “Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.
22
Kelele ya vita iko ndani ya nchi, kelele ya maangamizi makuu!
23
Tazama jinsi nyundo ya dunia yote ilivyovunjika na kuharibika! Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa miongoni mwa mataifa!
24
Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli, nawe ukakamatwa kabla haujafahamu; ulipatikana na ukakamatwa kwa sababu ulimpinga Bwana.
25
Bwana amefungua ghala lake la silaha na kuzitoa silaha za ghadhabu yake, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zote anayo kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo.
26
Njooni dhidi yake kutoka mbali. Zifungueni ghala zake za nafaka; mlundikeni kama lundo la nafaka. Mwangamizeni kabisa na msimwachie mabaki yoyote.
27
Waueni mafahali wake wachanga wote; waacheni washuke machinjoni! Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa.
28
Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli wakitangaza katika Sayuni jinsi Bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.
29
“Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli, wote wale wavutao upinde. Pigeni kambi kumzunguka kabisa, asitoroke mtu yeyote. Mlipizeni kwa matendo yake; mtendeeni kama alivyotenda. Kwa kuwa alimdharau Bwana, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
30
Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani; askari wake wote watanyamazishwa siku ile,” asema Bwana.
31
“Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,” asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, “kwa kuwa siku yako imewadia, yaani, wakati wako wa kuadhibiwa.
32
Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka, wala hakuna yeyote atakayemuinua; nitawasha moto katika miji yake, utakaowateketeza wote wanaomzunguka.”
Settings