Skip to content
Yeremia 48:14-28

Yeremia 48:14-28

14
“Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa, watu jasiri katika vita’?
15
Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa, vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.
16
“Kuanguka kwa Moabu kumekaribia, janga kubwa litamjia kwa haraka.
17
Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka, ninyi nyote mnaojua sifa zake, semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu, tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’
18
“Shuka kutoka fahari yako na uketi katika ardhi iliyokauka, enyi wenyeji wa Binti wa Diboni, kwa maana yeye aangamizaye Moabu atakuja dhidi yako, na kuangamiza miji yako iliyozungushiwa maboma.
19
Simama kando ya barabara na utazame, wewe unayeishi Aroeri. Muulize mwanaume anayekimbia na mwanamke anayetoroka, waulize, ‘Kumetokea nini?’
20
Moabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjavunjwa. Lieni kwa huzuni na kupiga kelele! Tangazeni kando ya Arnoni kwamba Moabu ameangamizwa.
21
Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu: katika Holoni, Yahasa na Mefaathi,
22
katika Diboni, Nebo na Beth-Diblathaimu,
23
katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli na Beth-Meoni,
24
katika Keriothi na Bosra; kwa miji yote ya Moabu, iliyoko mbali na karibu.
25
Pembe ya Moabu imekatwa, mkono wake umevunjwa,” asema Bwana.
26
“Mlevye, kwa kuwa amemdharau Bwana. Moabu na agaegae katika matapishi yake, yeye na awe kitu cha dhihaka.
27
Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa? Je, alikamatwa miongoni mwa wezi, kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau kila mara unapozungumza juu yake?
28
Ondokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba, enyi mnaoishi Moabu. Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chake kwenye mdomo wa pango.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options