Rukia maudhui
Isaya 26:1-8

Isaya 26:1-8

1
Katika siku ile, wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda: Tuna mji ulio na nguvu, Mungu huufanya wokovu kuwa kuta zake na maboma yake.
2
Fungua malango ili taifa lenye haki lipate kuingia, taifa lile lidumishalo imani.
3
Utamlinda katika amani kamilifu yeye ambaye moyo wake ni thabiti kwa sababu anakutumaini wewe.
4
Mtumaini Bwana milele, kwa kuwa Bwana, Bwana, ni Mwamba wa milele.
5
Huwashusha wale wajikwezao, huushusha chini mji wenye kiburi, huushusha hadi ardhini na kuutupa chini mavumbini.
6
Miguu huukanyaga chini, miguu ya hao walioonewa, hatua za hao maskini.
7
Mapito ya wenye haki yamenyooka. Ewe uliye Mwenye Haki, waisawazisha njia ya mtu mnyofu.
8
Naam, Bwana, tukienenda katika sheria zako, twakungojea wewe, jina lako na sifa zako ndizo shauku za mioyo yetu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options