Wagalatia 6:18
Inaonyesha mstari 18 pamoja na muktadha unaouzunguka.
15
Kwa maana katika Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa si kitu, bali kule kuwa kiumbe kipya ni kila kitu!
16
Amani na rehema viwe na wote wanaofuata kanuni hii, na juu ya Israeli wa Mungu.
17
Hatimaye, tangu sasa mtu yeyote asinitaabishe, kwa maana nachukua katika mwili wangu chapa zake Yesu.
18
Ndugu zangu, neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja na roho zenu. Amen.
Settings