Skip to content
Kutoka 12:23-28

Kutoka 12:23-28

23
Bwana apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu juu ya vizingiti na kwenye miimo ya milango, naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zenu na kuwapiga ninyi.
24
“Shikeni maagizo haya yawe kanuni ya kudumu kwenu na kwa ajili ya wazao wenu.
25
Mtakapoingia katika nchi Bwana atakayowapa kama alivyoahidi, shikeni desturi hii.
26
Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’
27
Basi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa Bwana, ambaye alipita juu ya nyumba za Waisraeli katika nchi ya Misri na hakudhuru nyumba zetu alipowapiga Wamisri.’ ” Ndipo watu wa Israeli waliposujudu na kuabudu.
28
Waisraeli wakafanya kama vile Bwana alivyomwagiza Mose na Aroni.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options