Rukia maudhui
Kumbukumbu 30:11-14

Amri ya Mungu Inapatikana kwa Urahisi

Kumbukumbu 30:11-14
11
Ninachokuagiza leo sio kigumu sana kwako au usichokiweza.
12
Hakiko juu mbinguni, ili uulize, “Ni nani atakayepanda mbinguni kukileta na kututangazia ili tuweze kutii?”
13
Wala hakiko ngʼambo ya bahari, ili uulize, “Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?”
14
La hasha! Lile neno liko karibu sana nawe; liko kinywani mwako na ndani ya moyo wako ili uweze kulitii.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options