Rukia maudhui

Zaburi28

Kilio cha Wokovu na Hukumu

1
Zaburi ya Daudi. Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu; usiwe kwangu kama kiziwi. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na walioshuka shimoni.
2
Sikia kilio changu unihurumie ninapokuita kwa ajili ya msaada, niinuapo mikono yangu kuelekea Patakatifu pa Patakatifu pako.
3
Usiniburute pamoja na waovu, pamoja na hao watendao mabaya, ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri, lakini mioyoni mwao wameficha chuki.
4
Walipe sawasawa na matendo yao, sawasawa na matendo yao maovu; walipe sawasawa na kazi za mikono yao, uwalipe wanavyostahili.
5
Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana, na yale ambayo mikono yake imetenda, atawabomoa na kamwe hatawajenga tena.

Ujasiri Unaotokana na Maombi Kujibiwa

6
Bwana asifiwe, kwa maana amesikia kilio changu nikimwomba anihurumie.
7
Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu, moyo wangu umemtumaini yeye, nami nimesaidiwa. Moyo wangu unarukaruka kwa furaha nami nitamshukuru kwa wimbo.

Maombi ya Wokovu wa Watu wa Mungu

8
Bwana ni nguvu ya watu wake, ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.
9
Waokoe watu wako na uubariki urithi wako; uwe mchungaji wao na uwabebe milele.
Use arrow keys to navigate
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options