Rukia maudhui

Zaburi140

Ombi la Wokovu Kutoka kwa Maadui Wenye Hila

1
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu; nilinde na watu wenye jeuri,
2
ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao, na kuchochea vita siku zote.
3
Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, sumu ya nyoka iko midomoni mwao.
4
Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu; nilinde na watu wenye jeuri wanaopanga kunikwaza miguu yangu.
5
Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa, wametandaza kamba za wavu wao, wametega mitego kwenye njia yangu.

Tamko la Kumtumaini Mungu na Ombi la Ulinzi

6
Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.” Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia.
7
Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu, unikingaye kichwa changu siku ya vita:
8
Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao, usiache mipango yao ikafanikiwa, wasije wakajisifu.

Ombi la Hukumu ya Mungu

9
Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe na shida zinazosababishwa na midomo yao.
10
Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! Na watupwe motoni, katika mashimo ya matope, wasiinuke tena kamwe.
11
Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi; maafa na yawawinde watu wenye jeuri.

Ujasiri Katika Haki ya Mungu

12
Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki, na kuitegemeza njia ya mhitaji.
13
Hakika wenye haki watalisifu jina lako, na waadilifu wataishi mbele zako.
Use arrow keys to navigate
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Reading Width 45 chars

Options